Mark 8:11-13

11 aMafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Isa. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12 bAkahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” 13Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo.

Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode

(Mathayo 16:5-12)

Copyright information for SwhKC